Wednesday, October 30, 2013

Tanganyikaone Habati za Kitaifa: TANZANIA KUAMUA KUJITOA EAC BAADA YA WIKI MBILI


Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inaangalia uwezekano wa kujitoa EAC kutokana na mataifa ya Kenya, Uganda na Rwanda kufanya vikao vya jumia hiyo bila kuishirikisha Tiaanzania na Burundi.

Serikali imewazuia mawaziri wawili kushiriki vikao viwili vya mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa madai kwamba imekuwa ikitengwa na baadhi ya nchi washirika wa EAC.

Akizungumzia sakata hilo bungeni mjini Dodoma waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta amesema waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe amezuiwa kwenda Kenya kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje unaoendela nchini humo huku naibu waziri wa masuala ya Afrika Mashariki akizuiwa na serikali asihudhurie mkutano utakaoanza hii leo Oktoba 31 nchini Burundi.


Waziri Sitta ameliambia Bunge kwamba baadhi ya nchi zinaonekana kuwa na shirikisho lao la Afrika Mashariki hivyo hakuna sababu ya mawaziri wake kuhudhuria vikao hivyo kwa sasa.

Waziri Sitta ametoa ufafanuzi huo Jumatano hii bungeni kufuatia mkutano uliofanyika hivi karibuni nchini Rwanda na kuwashirikisha marais wa Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan ya Kusini.

Akijibu hoja ya wabunge, kwa nini Tanzania isijitoe katika jumuiya hiyo waziri Sitta amewataka wawe na subira kwa muda wa wiki mbili wakati wanasubiri majibu ya msingi kutoka kwa sekretarieti ya jumuiya hiyo.

Jumuiya ya Afrika Mashariki inapita katika kipindi kigumu kutokana na kile kinachoonekana ni baadhi ya nchi wanachama kuitenga Tanzania katika baadhi ya mambo.

Pia washirika hao wanaamua kuitenga Tanzania baada ya kuona kuwa Tanzania inachelewesha mchakato wa kuanzisha shiriksho la Afrika mashariki baada ya tanzania kukataa baadhi ya vipengele ikiwa ni suala la umiliki binafsi wa ardhi na kutumia kitambulisho cha taifa kama hati ya kusafiria.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wandai kuwa utata huu umekuja pia baada ya Tanzania kupeleka jeshi kulinda amani katika nchi ya DRC ambao wanajeshi hao wanpigana na waasi wa M23 ambao inaaminika kuwa wanamafungamano na Serikali ya Rwanda.

Suala hilo limepelekea baadhi ya  wananchi na wanasiasa nchini kutaka nchi yao ijiondoe katika jumuiya hiyo.

No comments:

Post a Comment